RuvuShooting wanatarajia kuwakaribisha Wagosi wa Kaya (Coastal Union) katika mchezo wa raundi ya 5 wa NBC Primia Ligi baada ya ligi hiyo kusimama kwa takribani wiki mbili kufuatia kalenda ya FIFA.

 

RuvuShooting Kumkaribisha Coastal Union

 

RuvuShooting ambayo ipo chini ya kocha mkuu Boniphace Mkwasa wapo katika nafasi ya katikati ya ligi kuu ambayo ni nafasi ya saba, baada ya kucheza mechi nne, wakishinda mechi mbili, hawajapata sare na wamepoteza mechi mbili na wametoka kushinda mechi yao iliyopita dhidi ya Polisi Tanzania kwa bao moja 1-0.

Huku kwa upande wa Coastal Union mambo yakiwa magumu kwao kwani mpaka sasa wameuza wachezaji wao muhimu kwenda vilabu vingine, aliyekuwa kocha wao mkuu katimkia Simba na sasa wana kocha mpya ambae atakuwa anakionoa kikosi hicho ambacho makao makuu yake yapo Tanga Mkwakwani.

 

RuvuShooting Kumkaribisha Coastal Union

Coastal mpaka sasa toka msimu huu uanze ndani ya mechi nne, ameshinda mechi moja peekee ametoa sare moja na amepoteza michezo miwili, huku akishikilia nafasi ya 11 ambayo kwa ukubwa wake alionao hakupaswa kuwa kwenye nafasi hiyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa