Ali Kamwe afisa habari mpya wa klabu ya Yanga amefunguka kua klabu ya Yanga ni bora kuliko klabu ya Al-Hilal ya Sudani ambayo wanatarajia kucheza nayo siku za karibuni katika hatua ya pili ya ligi ya mabingwa Afrika.

Afisa habari huyo alieteuliwa hivi karibuni amezungumza mapema leo asubuhi akifanyiwa mahojiano na kituo cha Wasafi Fm akidai klabu ya Yanga kwasasa ni bora kuliko klabu hiyo ya Sudani kwa kila kitu kuanzia wachezaji wenye ubora,uwekezaji uliofanywa klabuni hapo pamoja kiwango kinachooneshwa na timu hiyo kwasasa.

ali kamweAli Kamwe ameeleza waandishi wa habari wengi wanajaribu kuwaogopesha mashabiki wa Yanga na kuwaaminisha kua klabu hiyo ya Sudani ni timu inayotisha na kusahau kuwaeleza ubora wa Yanga waliokua nao na kuwakumbusha waandishi hao kua timu hiyo haijapoteza michezo 41 ya ligi kuu mpaka sasa.

Ali Kamwe ameeleza timu ya Yanga kwasasa ina ubora wa hali ya juu na ndo timu bora kwasasa hapa Tanzania na kusema Al-Hilal ambao watacheza nao tarehe nane kwenye dimba la mkapa ni timu ambayo ni bora kihistoria ila kwa upande wa ubora kwasasa timu ya wananchi iko mbali sana.

ali kamweKamwe alimaliza kwa kusema kipindi wachokipitia Al-Hilal, Yanga walipita miaka minne nyuma kwakua amedai timu hiyo ya Sudani kwasasa inatengeneza timu wakati wao wana timu iliyo kamili na yenye ubora.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa