Nyota wa Arsenal, Emile Smith Rowe ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza.
Staa huyu mwenye miaka 21 ameungana na kikosi cha Uingereza pale St. George’s Park Jumatatu, katika maandalizi ya kuelekea jukumu la kimataifa la Kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Albania na San Marino.

Marcus Rashford, James Ward-Prowse, Mason Mount na Luke Shaw wameshindwa kuungana na kikosi hicho cha Uingereza kwa sabababu ya changamoto za maheraha.
Emile Smith Rowe, aliyetarajiwa kuungana na kikosi cha Vijana U21, ameungana rasmi na wenzake kutimiza ndoto yake ya kuchezea timu ya taifa, ambayo ni ndoto ya kila mchezaji anayecheza soka la kulipwa.
Smith Rowe amecheza mechi zote za Arsenal msimu huu, na ameweza kucheka na nyavu katika kila mechi kwenye mechi tatu za mwisho za ligi. Kuchaguliwa kwake ni zawadi ya kufanya vizuri kwenye ligi.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


