Enzo Fernandez ameweka malengo yake juu ya ubingwa wa Ligi kuu akiwa na Chelsea msimu huu baada ya kujiunga mnamo Januari, mshindi huyo wa Kombe la Dunia alivumilia mwanzo mbaya wa maisha Stamford Bridge huku The Blues wakichechemea nyumbani katika nafasi ya 12.
Lakini huku Muargentina mwenzake Mauricio Pochettino sasa akiwa ameshika usukani, Enzo ana imani kikosi kipya cha klabu yake kinaweza kupata tuzo kubwa zaidi katika soka la Uingereza wakati huu.
Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.
Akizungumza na tovuti rasmi ya Chelsea, Enzo alisema: “Lengo kuu mwaka huu ni kushinda Ligi Kuu. Sasa tuna kocha mkuu mpya, lazima useme matarajio yetu yamebadilika. Ni wazi, nilipofika, kila kitu kilikuwa kigumu. Kulikuwa na mabadiliko mengi na kila kitu kilifanyika haraka sana kwangu.”
Enzo amesema kuwa wanataka kuwa timu yenye ukali ambayo inashambulia na kulinda vyema, ambayo inaingia katika kila mchezo ili kushinda, bila kujali upinzani. Wanataka kutawala kila mchezo wanaocheza.
Chelsea wataanza kampeni yao ya ligi wakiwa nyumbani dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili.
Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. meridianbet.co.tz.
Wakati nyota aliyesajiliwa Christopher Nkunku huenda hatacheza kwa miezi kadhaa kutokana na jeraha, vijana hao wa Pochettino wamejawa na hali ya kujiamini baada ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.
Na Enzo mwenye miaka 22, anafurahia kufanya kazi chini ya mtani wake. Kuwa na kocha wa Argentina ni rahisi zaidi kwake. Kuzungumza naye, ni muhimu sana. Ni njia nyingine ya kuunganishwa kwa sababu bado hazungumzi Kiingereza kikamilifu, kwa hivyo kuzungumza naye kwa Kihispania ni rahisi zaidi.
Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.
Inasaidia kujiamini kwangu na ni uhusiano bora. Pia ina athari kubwa katika kujiamini kwangu. Ni muhimu sana kwangu kwamba Pochettino ameingia kwangu na wachezaji wenzangu. Atakuwa muhimu sana kwetu. Alisema mchezaji huyo.