Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano na klabu ya Brighton and Hove Albion kwajili ya kumchukua golikpa wa klabu hiyo Robert Sanchez kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 20.
Klabu ya Chelsea imeingia makubaliano na golikipa huyo mkataba wa muda mrefu ambao bado haujawekwa wazi, Lakini taarifa zinaeleza ni kua ni mkataba ambao utakua wa muda mrefu baina ya golikipa huyo na matajiri hao kutoka jiji la London.Robert Sanchez ni golikipa mwenye ubora mkubwa sana na amecheza ndani ya klabu hiyo kwa misimu kadhaa akiwa kwenye ubora mkubwa, Lakini anaondoka ndani ya klabu hiyo kwasasa baada ya Brighton kuridhia na kiasi kilichowekwa kimewashawishi.
Kocha Robert de Zerbi alianza kumuweka benchi golikipa huyo wa kimataifa wa Hispania, Huku ikielezwa ni kutokana na matatizo ya kinidhamu na sababu kubwa iliyochangia kumruhusu kuondoka ni baada ya kupata mbadala wake ambaye alicheza kwa kiwango bora.Klabu ya Chelsea inaonekana ni kama wameifanya Brighton mgodi wao kwani mpaka sasa walimeshamchukua Cucurela,aliyekua kocha wa klab hiyo Graham Potter, Robert Sanchez, na sasa bado wanafukuzia saini ya kiungo Moises Caicedo.