Simba Yaweka Rekodi Mauzo ya Tiketi

Klabu ya Simba imefanikiwa kuweka rekodi mpya ya kuuza tiketi zote kuelekea siku yao Jumapili ya tarehe 6 ambapo wamefanikiwa kufanya hivo siku tatu kabla ya tukio.

Simba imeshafanikiwa kujaza uwanja mapema zaidi katika sikukuu yao wakiwa walijaza uwanja mapema saa saba mchana, Kwasasa wamefanikiwa tena kwa mara nyingine kumpata baada ya kuuza tikite zote.simbaKlabu ya Wekundu wa Msimbazi wana jambo lao kubwa siku ya jumapili ambapo wiki hii nzima ilikua ni wiki ya hamasa kwa mashabiki wa klabu hiyo kuelekea Jumapli na wamefanikiwa kwani kabla ya siku ya tukio tiketi zimeisha.

Simba wametangaza kumaliza tiketi zote kuelekea kilele cha siku ya SIMBA DAY jumapili na hii inaonesha ukubwa wao kwenye kuandaa matamasha ya vilabu nchini kwani wao ndio walikua waanzilishi vilevile.simbaMpaka jana asilimia kubwa ya tiketi zilikua zimenunuliwa na klabu hiyo ilitoa wito kwa mashabiki wanunue tiketi maana mpaka kufikia leo huenda tiketi zingekua zimemalizika na ndio kilichotokea kwani jioni ya leo tiketi zimetangazwa kumalizika.

 

Acha ujumbe