Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani Hans Flick amesema kuwa lazima awajibike kwa kushindwa kwa timu yake katika michuano ya ligi ya Mataifa dhidi ya Hungary hapo jana baada ya kupoteza kwa bao 1-0.

 

Flick Anyanyua Mikono Juu.

Bao hilo moja lilifungwa na Adam Szalai kipindi cha kwanza ndilo pekee lililodumu hadi dakika 90 za kumalizika kwa mchezo huko Leipzig, na wenyeji Ujerumani wakashindwa kusawazisha bao hilo licha ya kumiliki mpira kwa kiwango kikubwa.

Vijana wa Hans Flick wamepoteza kwa mara ya kwanza dhidi ya Hungary tangu 2004 huku kikosi hicho cha Ujerumani mara nyingi kikiwa na wasiwasi licha ya udhibiti wao. Akizungumza baadae kocha huyo wa zamani wa Bayern Munich alikiri kuwa alicheza kamari kimakosa, ingawa kushindwa kwa England kutoka kwa Italia kunamaanisha kuwa wako salama kushuka daraja.

“Tulitaka kujaribu kitu na Jonas katika nafasi ya beki wa kulia”. Aliiambia ZDF. Lazima niwajibike kwa hilo. Hatukuwahi kufika pale tulipotaka kuwatumia mabeki wetu wa pembeni. Hiyo haikufanya kazi.

 

Flick Anyanyua Mikono Juu.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Flick alisema kuwa timu yake haitakatishwa tamaa na matokeo hayo huku kombe la Dunia likitarajiwa kupigwa huko Qatar mwaka huu. Ujerumani itarejea dimbani kumenyana na Uingereza ambayo tayari imeshuka daraja B ya ligi ya Mataifa katika uwanja wa Wembley Septemba 26.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa