Mshambuliaji wa Manchester City, Phil Foden amefanyiwa upasuaji kuondoa kidole tumbo hivyo hakucheza mechi ya Ukraine na pia ataikosa Liverpool Jumamosi.

Uingereza ilithibitisha habari hiyo hapo jana, na kumfanya Foden kutoshiriki mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Ukraine iliyomalizika kwa Three Lions kushinda 2-0.
City baadaye ilitangaza kwamba Foden bila shaka atakosa mechi muhimu ya Jumamosi ijayo ya Ligi kuu dhidi ya Liverpool.
Phil, ambaye aliingia kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa Uingereza dhidi ya Italia siku ya Alhamisi lakini alidumu kwa dakika 12 pekee, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa appendicitis.

Hakuna muda madhubuti uliotolewa wa kurejea kwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 22, ingawa mwongozo wa Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza (NHS) unapendekeza angalau kipindi cha wiki mbili cha kupona.
Phil amefunga mabao 13 na kutoa asisti tano katika mechi 36 alizoichezea City msimu huu.

