Foden Kuwakosa Woves Leo

Kiungo wa klabu ya Manchester City Phil Foden Kuwakosa klabu ya Wolverhampton katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza utakaopigwa katika dimba la Etihad.

Mchezaji huyo anakosekana katika mchezo huo baada ya kutumika katika mchezo wa katikati ya wiki dhidi ya klabu ya Tottenham ambapo Manchester City walipata ushindi wa mabao manne dhiidi ya mawili. Mpaka sasa taarifa haijatolewa juu ya kukosekana kwa mchezaji huyo.fodenMchezaji Phil Foden ambaye amekua kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ndani ya klabu ya Manchester City hivo kukosekana kwake katika mchezo wa leo inaweza kuonesha pengo kwa kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu hiyo.

 

Kukosekana kwa Phil Foden inaweza kuacha pengo ndani ya timu hiyo lakini urejeo wa kiungo fundi ndani ya Manchester City utaleta tabasamu kubwa kwani mchezaji huyo alikosekana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs.fodenManchester City leo watacheza nyumbani katika mchezo wao wa pili mfululizo dhidi ya klabu ya Wolves katika mchezo ambao utakua muhimu zaidi kwao, Kwani wakishinda watapunguza pengo la alama dhidi ya vinara klabu ya Arsenal mpaka kufikia alama mbili huku Arsenal wao wakiwa na mtihani mzito dhidi ya Manchester United.

Acha ujumbe