Klabu ya Real Madrid leo itashuka dimbani dhidi ya klabu ya Atletico Bilbao kwenye mchezo wa ligi kuu ya Hispania utyakaopigwa katika dimba la San Mames Barria.

Klabu ya Real Madrid watakwenda katika mchezo wa leo dhidi ya Bilbao huku wakikumbuka mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Hispania walipoteza dhidi ya Villarreal katika dimba la Estadio de Cerramica. Kutokana na hali hiyo inafanya mchezo kua tahadhari kubwa zaidi.Real MadridKlabu ya Atletico Bilbao mara ya mwisho wamecheza mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu ya Hispania walicheza dhidi ya mahasimu wao klabu ya Real Sociedad na kupoteza kwa mabao matatu kwa moja, Hivo watahitaji kupata matokeo katika mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi katika ligi hiyo.

Klabu ya Real Madrid wao wanataka kupata alama tatu muhimu ili kuwafikia wapinzani wao wakubwa katika ligi hiyo klabu ya Fc Barcelona ambao wao wanaongoza ligi kwa alama tatu, Kama Los Blancos watapata matokeo dhidi ya Bilbao ni wazi watakua wamewafikia klabu ya Barcelona ambao ndio vinara.Real MadridMabingwa watetezi hao nchini Hispania wataendelea kumkosa kiungo wao Aurelien Tchouameni ambaye anauguza majeraha ya mguu wake, Lakini wachezaji wengine wote watakuepo kuhakikisha klabu hiyo inapata alama tatu muhimu wakiwa ugenini katika dimba la San Mames Barria.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa