Klabu ya Real Madrid inaelezwa haipo kwenye mpango wa kumuachia mchezaji wa klabu hiyo Eduardo Camavinga ambaye inaelezwa klabu ya Arsenal inamnyatia kwenye dirisha hili dogo la mwezi Januari.

Klabu ya soka ya Arsenal inaelezwa ipo kwenye mpango wa kumnasa kiungo huyo ndani ya majira haya ya baridi kwa mkopo ili kuimarisha safu ya kiungo ya klabu hiyo, Lakini taarifa kutokana nchini Hispania klabu ya Real Madrid haina mpango wa kumuachia mchezaji huyo.Real MadridEduardo Camavinga ambaye amekua mchezaji anaetokea nje muda mwingi kwenye michezo ya Real Madrid na kufanya vizuri pale anapokua anaingia, Ilionekana kama klabu hiyo ingekubali kumuachia mchezaji huyo ili akapate nafasi ya kucheza mda mrefu ndani ya klabu ya Arsenal lakini imekua tofauti.

Wakala wa mchezaji Camavinga alitoa ufafanuzi juu ya taarifa ya kua mchezaji wake anataka kujiunga na klabu ya Arsenal kwa mkopo ili akapate nafasi ya kucheza mda mrefu ambayo amekua hapati ndani ya timu hiyo, Lakini wakala huyo amekanusha na kusema mchezaji huyo bado yupo sana ndani ya klabu na ana furaha kuwepo hapo na habari hizo hazina ukweli wowote.Real MadridKlabu ya Real Madrid inamchukulia Camavinga kama wachezaji wasiogusika ndani ya klabu hiyo kutokana na kipaji chake, Pia ni mchezaji ambaye anatizamiwa kua kwenye kikosi cha klabu hiyo kwa muda mrefu na kutengeneza kizazi bora zaidi kutoakana pia na umri wake mdogo ambao anao kwasasa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa