Liverpool, Chelsea Hakuna Mbabe

Klabu ya Liverpool na Chelsea ambazo zimekutana katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza na mchezo huo kumalizika kukiwa hakuna mbabe baada ya kutoka suluhu.

Klabu ya Liverpool ambayo ilikua nyumbani imeshindwa kutumia faida ya kua nyumbani kuweza kupata matokeo dhidi ya klabu ya Chelsea ambao walikua wageni. Mchezo huo ulikua wenye upinzani mkali kwani kila mmoja alitamani kupatya matokeo dhidi ya mwenzake kutokana na hali zao katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.liverpoolKlabu ya Chelsea ilifanikiwa kupata bao la mapema tu dakika ya tatu ya mchezo kupitia kwa mchezaji Kai Harvertz lakini bao hilo lilikataliwa baada ya kuonekana mchezaji Thiago Silva alikua ameotea. Mchezo huo uliendelea mpaka kwa kutafuta baina ya timu zote mbili lakini mpaka mapumziko hakuna aliefanikiwa kuona lango la mwenzake.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini bado hawakuweza kufungana mpaka dkika tisini za mchezo zinamalizika, Japo klabu ya Chelsea ilionekana kuutawala mpira zaidi ya wenyeji klabu ya Liverpool waliokua wenyeji wa mchezo huo.liverpoolKlabu zote mbili zimeendelea kusalia nafasi zilizokuepo kwani wamefanikiwa kuongeza alama moja klabu ya Liverpool wao wakiwafanikiwa kufikisha alama 29 wakiwa nafasi ya nane kwenye msimamo, Huku klabu ya Chelsea wao wakiwa nafasi ya 10 wakiwa na alama zao 29 pia wakiwa wanazidiwa na Brentford walio nafasi ya tisa na Liverpool nafasi ya nane kwa tofauti ya magoli.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.