Moukoko Ajifunga Dortmund Mpaka 2026

Kinda wa kimataifa wa Ujerumani Youssoufa Moukoko anayekipiga klabu ya Borussia Dortmund amejifunga ndani ya klabu kwa kuongeza mkataba mpya utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2026.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 tu ameamua kusalia ndani ya klabu ya Borussia Dortmund akiongeza mkataba wa miaka mitatu na nusu ambao utamuweka kwenye viunga vya Signal Iduna Park mpaka mwaka 2026.

Moukoko ambaye makataba wake ulikua unaelekea ukingoni mwisho mwa msimu huu na kuna vilabu kadhaa barani ulaya vilikua vinawinda saini ya kinda huyo mwenye kipaji kikubwa. Klabu ya Borussia Dortmund wamefanikiwa kumbakiza kinda huyo klabuni hapo mpaka majira ya kiangazi mwaka 2026.

Kinda Moukoko licha ya kutambua kuna vilabu vingi vinahitaji saini yake lakini hakusita kuonesha mapenzi yake na klabu ya Borussia Dortmund,  Na kueleza anaipenda klabu hiyo kwani amecheza klabu hiyo tangu timu za vijana na anajiskia amani ndani ya timu hiyo pamoja na kuaminiwa na benchi la ufundi lakini pia anasema ndio sehemu sahihi anaweza kukua zaidi kimpira.

Mshambuliaji Youssoufa Moukoko ambaye alipata kashafa ya kudanganya umri siku kadhaa nyuma ameweza kusaini mkataba mpya na klabu hiyo na kuongeza idadi ya wachezaji vijana wenye ubora mkubwa ndani ya Borussia Dortmund akiambatana na wachezaji kama Karim Adeyemi, pamoja na kiungo wa kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.