Simba Kuwakosa Wachezaji Kumi Leo

Klabu ya Simba leo itashuka dimbani leo dimbani kumenyana klabu ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC ambapo itawakosa wachezaji wake kumi katika mchezo wake.

Klabu hiyo ambayo itakua mgeni katika dimba la Jamhuri ikimenyana na Dodoma Jiji kutafuta alama tatu muhimu lakini inakabiliwa na majeruhi kibao na wachezaji wengine ambao wameadhibiwa na wataukosa mchezo huo muhimu wa ligi ya NBC.simbaKlabu ya Simba leo itawakosa Moses Phiri, Pape Ousmane Sakho, Henock Inonga, Peter Banda, Clatous Chama, Jonas Mkude, Israel Mwenda hawa ni ni wachezaji saba ambao wataukosa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji kutoka na kuandamwa na majeraha.

Wachezaji wengine watatu ambao watakosekana katika mchezo huo ni Mzamiru Yassin, Saidio Kanoute, na Joash Onyango hawa watakosekana kutokana na kutumikia adhabu baadda ya kupata kadi tatu za njano ambapo kutokana na kanuni hawataweza kucheza mchezo huo.simbaKlabu ya Simba rekodi inawabeba wanapokutana na klabu ya Dodoma Jiji tangu klabu hiyo ipande ligi kuu imekutana na mnyama mara tano huku ikipoteza michezo yote mitano na huu wa leo ni mchezo wa sita, Hivo inasubiriwa kama Simba itaendeleza ubabe wake dhidi ya Dodoma Jiji.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.