Simba Yaifuata Dodoma Jiji

Klabu ya soka ya Simba imeondoka jijini Dar-es-salam leo kuelekea mkoani Dodoma ili kwajili ya kwenda kumenyana na klabu ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Baada ya kuifunga klabu ya Mbeya City na kuchukua alama tatu muhimu sasa nguvu wanaelekeza katika mchezo unaofuata dhidi ya Dodoma Jiji, Ambapo klabu hiyo imeondoka leo kuelekea mkoani humo ambapo mchezo utapigwa siku ya jumapili katika dimba la Jamhuri jijini Dodoma.simbaWekundu wa msimbazi wako kwenye opereshni maalumu ya kuhakikisha wanaurejesha ubingwa walioupoteza mbele ya watani zao klabu ya Yanga msimu uliomalizika. Klabu hiyo mpaka sasa imeachwa jumla ya alama sita na klabu ya Yanga lakini wana imani wanaweza kurejesha taji hilo mitaa ya msimbazi.

Kocha wa mpya wa klabu ya Simba Roberto Oliviera maarufu kama Robertinho atakua na kibarua cha pili cha kuiongoza klabu hiyo katika mchezo wa pili wa ligi kuu ya NBC baada ya kufanikiwa kushinda mchezo wa kwanza dhidi ya klabu ya Mbeya City.simbaKlabu ya Simba itawakosa baadhi ya nyota wake katika mchezo huo dhidi ya klabu ya Dodoma Jiji siku ya jumapili ambao ni Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute, pamoja beki Joash Onyango ambao wana kadi tatu za njano hivo kikanuni hawataruhusiwa kucheza mchezo huo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.