Klabu ya Tottenham ipo kwenye mchakato wa kuhakikisha inanasa saini ya mchezaji Nicolo Zaniolo anayekipiga katika klabu ya AS Roma kutoka nchini Italia kwa mkopo.
Klabu ya Tottenham kwasasa inakonekana kupitia kipindi kigumu ambapo imekua haipati matokeo ya kuridhisha chini ya mwalimu Antonio Conte, Hivo inataka kuingia sokoni Januari hii na kuimarisha kikosi chake kuelekea ungwe ya pili ya msimu huu.
Klabu hiyo inataka kumchukua kiungo Nicolo Zaniolo kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu huu huku wakitaka kuwepo na kipengele cha kumnunua moja kwa moja kiungo huyo fundi wa kimataifa wa Italia. Zaniolo ambaye anatajwa kama moja ya viungo wenye umri mdogo mafundi zaidi kutoka nchini Italia.
Klabu ya As Roma wao wanahitaji klabu ya Tottenham wamnunue jumla kama wanamuhitaji mchezaji huyo na sio kumchukua kwa mkopo, Lakini vijogoo hao wa London wao wanahitaji saini ya mchezaji huyo kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu na ikitokea wakaridhidhwa nae ndio watamchukua kwa mkataba wa kudumu.
Klabu ya Tottenham inasubiri maelekezo kutoka kwa klabu ya AS Roma kuangalia kama watakubali kumuachia mchezaji huyo kwa mkopo, Lakini kama AS Roma watagomea ofa hiyo basi vijogoo wa London watahitaji kutafuta mchezaji mwingine haraka ili kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao.

