Gian Piero Gasperini aliwapa zawadi maalum mashabiki wa Atalanta waliosafiri kwenye uwanja wa Anfield, akiwarushia koti lake baada ya ushindi wa 3-0 wa robo fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Liverpool.
Zaidi ya wafuasi 2,000 walifunga safari kuelekea Merseyside kwa mechi hiyo jana usiku lakini hata wao pengine hawakutarajia matokeo na uchezaji wa ajabu kama huo kutoka kwa La Dea.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Gianluca Scamacca alifunga mabao mawili kabla ya Mario Pasalic kufunga kwa mpira uliorudi kutoka kwa golikipa aliyechanganyikiwa na kukamilisha kipigo cha 3-0.
Ni mechi ya kwanza pekee na atakayeamua atakuwa Bergamo Alhamisi ijayo, lakini wakati wa sherehe, Gasperini alirusha koti lake pembeni mwa umati ili kumpa mtu kipande cha historia ya Calcio.