Christian Pulisic: “Inakatisha Tamaa, Lakini Sitapaniki Kuhusu Ukame wa Mabao AC Milan na USA."

Christian Pulisic anakiri kuwa amekuwa akipitia kipindi kigumu akiwa na AC Milan pamoja na timu ya Taiaf ya Marekani , lakini anaamini mpira utagonga goti lake na kuingia wavuni, na mambo yatabadilika.

Christian Pulisic: “Inakatisha Tamaa, Lakini Sitapaniki Kuhusu Ukame wa Mabao AC Milan na USA."

Mshambuliaji huyo alikuwa kwenye kiwango cha kushangaza mwaka 2025, lakini hajafanikiwa kufunga bao lolote kwa AC Milan katika mwaka huu wa kalenda, jambo linaloongeza ukame wake wa kimataifa unaoendelea tangu 2024.

Alipata tena usiku mgumu wakati Marekani  walipokuwa wakijiandaa kwa jukumu lao la kuwa wenyeji wa FIFA World Cup 2026 majira ya joto, ambapo walipoteza nyumbani kwa mabao 5-2 dhidi ya Ubelgiji.

“Kwangu mimi inakatisha tamaa. Ninahisi ningeweza kufanya vizuri zaidi kwenye moja ya nafasi. Niliikosa, halafu wao wakaenda kufunga, na mchezo ukabadilika. Inanikera sana, bila shaka.” Christian Pulisic aliwaambia waandishi wa habari.

Nafasi hiyo ilikuwa pale alipoupiga mpira juu ya lango wakati matokeo yalikuwa 1-1, na muda mfupi baadaye Ubelgiji wakachukua uongozi wa 2-1.

Sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anajaribu kubaki na mtazamo chanya licha ya changamoto anazokutana nazo mbele ya lango, akiwa na AC Milan pamoja na timu ya Marekani.

Christian Pulisic: “Inakatisha Tamaa, Lakini Sitapaniki Kuhusu Ukame wa Mabao AC Milan na USA."

“Imekuwa kipindi kigumu, lakini ninajiamini kwa namna ninavyocheza. Ninajisikia vizuri na ninatengeneza nafasi. Kwa hiyo ninatakiwa kubaki chanya na kuendelea mbele. Lakini ndiyo, ninahitaji kuwa makini zaidi katika nyakati hizo.”

Christian Pulisic anatumaini kwamba msemo wa zamani kuhusu mabao kuwa kama chupa ya ketchapu kwamba mara kizuizi kikiondoka na mtiririko kuanza, basi hautasimama utakuwa kweli kwake. Anachohitaji ni bahati kidogo tu, ambayo kila mshambuliaji huitaji wakati fulani katika maisha yake ya soka.

“Najua kuna siku mpira utagonga goti langu na kuingia wavuni, na mambo yatabadilika. Kwa hiyo sitapaniki  ni bora haya yatokee sasa kuliko majira ya joto. Mambo yatabadilika.”

Hata hivyo, ameweza kufunga mabao 10 na kutoa pasi za mabao 3 katika mechi 27 rasmi kwa AC Milan msimu huu, lakini yote yalifungwa kabla ya Mwaka Mpya.

Christian Pulisic hajafunga bao lolote katika  tangu ushindi wa 3-0 dhidi ya Hellas Verona

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.