De Gea Aipatia Fiorentina Pointi 3

Bila shaka, De Gea anatajwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi baada ya kuokoa penalti mbili katika ushindi wa 2-1 wa Fiorentina, lakini hataki kujipongeza kwa hilo.

De Gea Aipatia Fiorentina Pointi 3

Ulikuwa usiku usio wa kawaida katika Uwanja wa Artemio Franchi, kwani kulikuwa na penalti tatu zilizopigwa mbili na De Gea kwa Theo Hernandez na Tammy Abraham, nyingine na Mike Maignan juu ya Moise Kean.

Adli pia alifunga dhidi ya klabu yake kuu, wakati Christian Pulisic alifunga voli ya ajabu kutoka pembe ngumu zaidi, lakini Albert Gudmundsson alifunga bao la ushindi.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

De Gea Aipatia Fiorentina Pointi 3

Hakutakuwa na shaka yoyote kuhusu tuzo ya MOTM, kwani De Gea alikua kipa wa kwanza tangu Federico Marchetti akiwa Carpi-Lazio mnamo Mei 8, 2016 kuokoa penalti mbili kwenye mechi moja ya Serie A.

Lakini, Mhispania huyo mkongwe hakuwa na nia ya kuchukua sifa hiyo.

“Ni usiku wa ajabu. Tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii kwa miezi kadhaa, ningependelea kuzungumzia hilo zaidi ya kuokoa penalti, kwani tulitaka kuwafurahisha mashabiki,” De Gea aliambia DAZN.

Ushindi wa jana ni muhimu sana dhidi ya klabu kubwa kama Milan. Wanafanya kazi kwa bidii na mwishowe inaanza kuleta matunda. Alisema mchezaji huyo.

De Gea Aipatia Fiorentina Pointi 3

Zimekuwa ni siku chache ajabu kwa Adli, ambaye alifunga kwenye Conference league dhidi ya The New Saints siku ya Alhamisi, kisha akafunga bao dhidi ya klabu yake kuu usiku wa jana.

“Leo ilikuwa mchezo maalum kwangu, hakika. Ninaipenda sana klabu hii na nilitaka kufanya vyema. Zaidi ya yote nina furaha kwa timu, ambayo inafanya kazi kwa bidii na tulistahili kurudisha pointi tatu nyumbani,” Adli aliiambia DAZN.

Kiungo huyo, ambaye yuko kwa mkopo kwa gharama ya €1.5m na chaguo la Fiorentina kumnunua kwa €10.5m nyingine, alikataa kusherehekea dhidi ya Milan.

De Gea Aipatia Fiorentina Pointi 3

“Ni upendo na pia heshima, jinsi nimekuwa nikitendewa kwa miaka michache iliyopita. Bado nina marafiki, kaka na mashabiki huko, kwa hivyo hakuna kitu zaidi ya upendo.”

Acha ujumbe