Wakala wa Simone Inzaghi alikutana na wakurugenzi wa Inter jana na mazungumzo yanaendelea kwa kandarasi mpya na iliyoboreshwa baada ya ushindi wake wa Scudetto.

Kocha huyo alichukua mikoba ya Antonio Conte msimu wa joto wa 2021 na mkataba wake wa sasa utaendelea hadi Juni 2025. Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Alishinda taji la Serie A, matoleo matatu ya Supercoppa Italiana, makombe mawili ya Coppa Italia na kufika Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Yote yalitosha kumpatia Inzaghi mwenye umri wa miaka 48 mshahara ulioboreshwa, lakini bado kuna baadhi ya maelezo ya kusuluhishwa.


