Coastal Union Wamshusha Djuma Shaban

Klabu ya Coastal Union yadaiwa kukamilisha usajili wa beki wa zamani wa klabu ya AS Vita na Yanga Djuma Shaban.

Coastal imemsajili nyota huyo kama mchezaji huru baada ya kupita msimu mzima bila kuwa na timu ya kuitumikia.

Haya ni maandalizi ya klabu ya Coastal Union kuelekea mashindano ya kombe la shirikisho Barani Afrika msimu ujao.

Kocha Juma Mgunda ndiye anayetajwa kumtaka mchezaji huyo Ili kuongeza uzoefu kwenye eneo la ulinzi Kwa ajili ya Mashindano ya Kimataifa.

Acha ujumbe