BAADA ya kuachana na kocha Mwinyi Zahera Klabu ya Coastal Union imetangaza ujio wa Kocha mpya David Ouma atakayeinoa klabu hiyo.

Uongozi wa klabu ya Coastal Union kupitia kwa msemaji wao Abbas Mwamba alisema: “Karibu sana mwalimu wa viwango, mwalimu wa mafanikio, mwalimu wa technics, ubora wa elimu na kiwango chako ndio tunajivunia. Experience kutoka kituo Cha Ajax Amsterdam,Leseni ya UEFA, Leseni CAF A.

“Kocha msaidizi timu taifa ya Kenya chini Bobby WilliamsUmelitawala soka kenya kwa zaidi ya miaka 21 kupitia,pasta rangers,sofapaka, na legend wa madare utd”

“Karibu sana coach wa mafanikio. Wanamangushi Wana Imani kubwa sana na wewe” Kiongozi wa Coastal Union akimkaribisha kocha huyo



JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa