Kocha wa Viungo Yanga Atimka

ALIYEKUWA mtaalamu wa Viungo Yanga, Youssef Ammar amefunguka kuondoka katika klabu hiyo, hivyo hatakuwa sehemu ya Benchi la Ufundi la timu hiyo.

Akizungumza na Meridian Sports Youssef alisema kuwa anaondoka Yanga, kutokana na shinikizo la Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi, ambaye ameshinikiza kwenda kwa uongozi na kuwaambia anapaswa kuachwa.

Aliongeza kuwa kwa sasa hawezi kuweka wazi kila kitu, lakini yeye hawezi kubembeleza mtu au kumuabudu mtu. Huku akisema yeye ni mtu mweledi kwenye kazi yake.

“Kuna uwezekano mkubwa nikaondoka Yanga, lakini Sababu kubwa ikiwa ni Kocha Gamondi, sielewi nini shida lakini yeye ameutaka uongozi niondoke.

“Nipo tayari kuondoka kama viongozi watakuwa tayari Kwa Hilo na siwezi kumsujudia mwanadamu Kwa Sababu ya kazi,” alisema.

Mpaka Sasa hakuna taarifa yoyote kutoka Kwa uongozi wa Yanga, licha ya Meridian Sports kuingia chimbo kusaka habari hiyo bado limegonga Mwamba.

Acha ujumbe