MWENYEKITI wa Klabu ya Simba Murtaza Mangungu, ameamua kukata mzizi wa fitina na kusema kuwa yeye atabaki Simba na hataondoka licha ya shinikizo kuwa kubwa.
Akizungumza na Meridian Sports Mangungu alisema, ameona Kila kitu na anasikia vita ambayo anapigwa na mashabiki, lakini Kwa bahati mbaya hawajui nini kinaendelea na yeye siyo chanzo cha matatizo.
Huku akisema Kila kitu ambacho alisema Mjumbe wa Klabu hiyo CPA Issa Masoud hakina uhalisia na ukweli wowote.
“Sisi tunajuana tangu tunakua , haiwezekani mtu ambaye hana nasaba na Simba akawa ndani ya klabu , mimi nimepata kadi yangu ya uwanachama mwaka 1993”
“Niulize sasa , Kwahiyo tangu mwaka 1993 tuseme nilijipanga nije kuwa mwemyekiti wa Simba ili nije kuihujumu ? anayenishutumu mimi nahujumu Simba yeye hata kadi ya uanachama hana”
Wakati anajibu kuhusu maoni ya mdau aliyehoji viwango duni vya baadhi ya wachezaji wanaosajiliwa na Simba Mangungu amesema.
“Yeye amezungumzia wachezaji wawili Sawadogo na Jobe , bahati mbaya Sawadogo wakati anakuja pre season aliumia , lakini alikuwa anatoka kwenye timu yao ya Taifa sio mchezaji wa kiwango kidogo”