Mangungu Amkataa Hadharani Mo, Ajibu Msimamo Wake

MWENYEKITI WA SIMBA, Murtaza Mangungu ameweka msimamo wake juu ya Mohammed Dewji kurejea katika nafasi ya Salim Abdallah Try Again, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu hiyo. Jisajili na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo 1000+

Mangungu kupitia kituo cha ITV alizungumzia juu ya maamuzi hayo ya bodi, huku kwa upande wake akiweka ngumu kukubali maamuzi hayo, ambayo yamemfaya muwekezaji wa timu hiyo Mohammed Dewji kurejea Lunyasi.

“Suala la Try Again kujiuzulu na kumpendekeza MO kuwa Mwenyekiti wa Bodi ni maoni yake binafsi nje na utaratibu wa Kikatiba, Mwenyekiti wa Bodi anachaguliwa na Wajumbe wa bodi kwa kupigiwa kura hivyo tutamchagua Mwenyekiti wa Bodi kwa mujibu wa Katiba”- Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu.

Hata hivyo Mangungu ameenda mbali zaidi na kusema kwamba, yeye binafsi upo tayari kutoa pesa ya usajili, bila kumtegemea Mo Dewji. Beti na Meridianbet kwa uhakika wa ushndi wako.

“Pesa za usajiri niko tayari kutoa mwenyewe kwa kushirikiana na wanachama na wapenzi wa Simba, kwa sasa natafuta Mkurugenzi wa ufundi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia mtandao wa usajili na upembuzi wa kina kabla ya mchezaji kusajiliwa.”

Akizungumzia juu ya wajumbe waliojiuzulu, amesema kwamba wajumbe wengine watateuliwa upande wa muwekezaji, na kisha mchakato wa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Bodi utaanza.

“Hakuna wasiwasi wowote wa Wajumbe ambao wameamua kujiuzulu kwasababu wamejipima na wameona wanahitaji changamoto mpya, hivyo Wajumbe wengine watateuliwa upande wa Mwekezaji, waje tuchague Mwenyekiti mpya wa Bodi na tufanye kazi”

Acha ujumbe