PSG Waliwachukulia Poa Man Utd -Kimpembe

 

Wakati PSG wakiwa wanaendelea kuuguza jeraha lao la kutemwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu baada ya kuchapa bao 1-3 wakiwa nyumbani, Presnel Kimpembe anasema kuwa kuchapwa kwao imekuwa ishu ya kisaikolojia na kuwachukulia poa Manchester United.

Wakati Man Utd wakijitengenezea historia ya klabu ya kwanza kuweza kuchomoka kuingia hatua inayofuata ya Ligi Mabingwa Ulaya baada ya kupokea kichapo cha bao kuanzia 2 wakiwa nyumani, PSG wao wamejitengenezea historia ya kuwa klabu ya kwanza kushindwa kusonga mbele baada ya kushinda gemu ya ugenini kwa bao kuanzia 2 kuendelea.

Bila shaka mabingwa hawa wa Ligue 1 hawakutaka kutengeneza historia hii, ila wamejikuta tu wamepatikana na kasheshe hilo. Hii sio mara ya kwanza kwa mabingwa hawa kupata matokeo ya ajabu, inakumbukwa miaka 2 iliyopita pia waliweza kumchapa Barcelona bao 4-0 wakiwa nyumbani na wakapinduliwa kwenye gemu ya pili kwa kuchapwa bao 6-1 pale Camp Nou.

Kwa mujibu wa Kimpembe anaamini klabu yake ilikosean kujiaminisha kuwa kazi ilikamilika walipokuwa Old Trafford, wakidhani kuwa wasingeweza kupoteza wakiwa nyumbani, lakini mambo yakawageukia.

Kimpembe aaamini kuwa wamewaumiza mno mashabiki wao na kwa upande wake anaweza kuonja radha ya machungu ambayo wanayo mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo Kimpembe analaumiwa na baadhi ya wachezaji wenzake kwa kusababisha goli la penati. Lukaku alibaki kumfariji nyots huyu baada ya kupoteza gemu hivyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.