Mshambuliaji wa Real madrid Karim Benzema ameondolewa kwenye kikosi ambacho kinasafiri dhidi ya Rayo Vallecano hii leo  ambayo inaweza kuwa ishara ya wasiwasi kwa Ufaransa kabla ya Kombe la Dunia.

 

Benzema Kuwakosa Vallecano Leo

Mshindi huyo wa Ballon d’Or alirejea kutoka kwa mapumziko mafupi na kucheza akitokea benchi katika ushindi wa mabao 5-1 wa Madrid dhidi ya Celtic kwenye Ligi ya Mabingwa siku ya Jumatano lakini sasa amerejea nje ya uwanja.

Benzema amepata hitilafu ya misuli kwenye sehemu zake za chini za mguu wa kushoto na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 bado hajatulia, ingawa kocha mkuu wa Madrid Carlo Ancelotti anatarajia kuwepo kwa mechi yao ya nyumbani dhidi ya Cadiz siku ya Alhamisi.

Benzema Kuwakosa Vallecano Leo

Benzema anaungana na beki Antonio Rudiger kukosa mchezo wa leo huku  Madrid wakitafuta ushindi ambao utawarudisha juu ya Barcelona kileleni mwa LaLiga, na Carlo amesema kuwa Karim hatacheza kwasababu hajisikii sawa.

Kocha anaongeza kuwa alionekana kwamba yupo sawa, lakini anajitahidi kidogo na hatapatikana kesho . Dhidi ya Cadiz hadahani kama Rudiger atarejea, lakini Karim huenda akawepo.

Benzema ameanza mechi 11 pekee katika mashindano yote msimu huu, akifunga mabao sita. Alifunga mabao 44 katika mechi 46 msimu uliopita, kiasi cha kutosha kushinda tuzo ya Ballon d’Or yenye thamani kubwa, na kumweka kama mchezaji bora wa soka duniani katika kampeni za 2021-22.

Benzema Kuwakosa Vallecano Leo

Ancelotti pia aliulizwa kuhusu ulinganisho kati ya Rodrygo na nguli wa Brazil Ronaldo lakini anasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ananufaika na ubora unaomzunguka Santiago Bernabeu.

“Ronaldo hakuwa na bahati kama Rodrygo,” Ancelotti alisema. “Hapo zamani, Real Madrid hawakuwa na nguvu kama ilivyo sasa kwenye Ligi ya Mabingwa, Rodrygo anaweza kufaidika zaidi na hilo ikiwa atafikia viwango vya Ronaldo kwa mtu binafsi, tutakuwa tunamjengea sanamu.”


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa