Sadio Mane anaiunga mkono timu yake ya Senegal kwa kuwaambia wahezaji wenzake waonyeshe kiwango cha hali ya juu katika mechi ya kwanza ya ufunguzi ambapo watakuwa wakimenyana dhidi ya Uholanzi majira ya saa 1:00.

 

Mane Aiambia Senegal Waonyeshe Kiwango Chao

Mshambuliaji huyo wa Bayern Munich Mane alitarajiwa kuongoza harakati za timu hiyo nchini Qatar, lakini kutokana na jeraha baya la mguu limemfanya akose kushiriki michuano hiyo.

Kwenye karatasi, inaonekana timu imedhoofika sana kwa kukosekana kwake, lakini Mane anasema ukweli unaweza kuwa tofauti, akiunga mkono kundi aliloacha kukabiliana na changamoto yao.

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool aliandika kwenye Instagram: “Jumatatu hii, nchi yetu pendwa itashiriki Kombe la Dunia, Qatar 2022. Nina hakika Senegal itavuka na kukaribia kila mchezo kama fainali ya kweli.”

Mane Aiambia Senegal Waonyeshe Kiwango Chao

Mane aliongeza kwa kusema kuwa ana uhakika kwamba Wanasenegal wote watakuwa mbele ya skrini ndogo kuunga mkono na kuhimiza timu yao ya Taifa shujaa. Kama wafuasi wote wa ‘Taniere’, ana uhakika kwamba wachezaji wenzake watapigana kama mtu mmoja na kama wanavyofanya ili kuliheshimisha Taifa.

Simba wa Teranga walitinga robo fainali kwa kushangaza wengi mwaka wa 2002, na kama mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika walizingatiwa na wengi kama tumaini kuu la bara la Afrika kwa mafanikio ya Kombe la Dunia wakati huu.

Kukosekana kwa Mane ambae ana kunaweza badilisha mtazamo kwa watu wengi. Lakini mchezaji huyo hataweza kucheza baada ya kuumia kwenye mchezo wao wa Bundesliga akiwa na Bayern na  kuondolewa kwenye kikosi cha Senegal, na anaweza kukaa nje miezi kadhaa.

Mane Aiambia Senegal Waonyeshe Kiwango Chao

Mane aliwashukuru watu waliomtakia heri na kuandika: “Wengi wenu mmetuma ujumbe wa kuniunga mkono kufuatia kuumia kwangu. Namshukuru Mungu, upasuaji nilioupata katikati ya wiki ulikwenda vizuri. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwashukuru ninyi nyote.”


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Mane, Mane Aiambia Senegal Waonyeshe Kiwango Chao, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa