Mchezaji wa Fulham Aleksandar Mitrovic anasalia kuwa shakani kucheza  Kombe la Dunia licha ya kutajwa katika kikosi cha wachezaji 26 cha Serbia, kulingana na kocha mkuu wa Fulham Marco Silva.

 

Mitrovic Shakani Kulivaa Kombe la Dunia

Mshambuliaji huyo amefunga mabao tisa katika mechi 12 za Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na Fulham msimu huu, lakini alikosa mechi ya wiki iliyopita ambayo waliyofungwa 2-1 na Manchester City kutokana na jeraha.

Jeraha hilo linatarajiwa kumfanya Mitrovic kutoshiriki mechi ya hapo kesho ya nyumbani dhidi ya Manchester United, na mechi hiyo ndiyo itakuwa ya mwisho kwao kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia.

Mitrovic alijumuishwa kwenye kikosi cha Dragan Stojkovic siku ya Ijumaa, lakini Silva aliweka wazi kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 bado anahitaji uchunguzi zaidi wa kimatibabu kabla ya kuruhusiwa kushiriki Qatar.

Mitrovic Shakani Kulivaa Kombe la Dunia

Silva alisema; “Ninachoweza kukuambia ni kwamba itakuwa uamuzi utakaofanywa pengine katika siku za kwanza za wiki ijayo, kati ya wafanyakazi wa matibabu wa Serbia na wafanyakazi wetu wa matibabu.”

Na hiyo itasaidia kuamua ni uamuzi gani bora kwake, na kwao kama klabu pia kwasababu yeye ni muhimu sana. Aliongeza kwa kusema kuwa anachojua yeye kwasasa ni kwamba hakuwa tayari kwa mechi iliyopita na hatakuwa tayari kwa mechi inayofuata.

Mitrovic amefunga mabao 50 katika mechi 76 alizoichezea Fulham, yakiwemo mabao nane kati ya matano katika kampeni ya nchi yake ya kufuzu kwa Kombe la Dunia, mshambuliaji huyo anataka kuwa kwenye Kombe la Dunia. Alitaka kuwepo Jumapili hapa dhidi ya Man United, na alitaka kucheza dhidi ya City.

Mitrovic Shakani Kulivaa Kombe la Dunia

Serbia wanashiriki Kombe lao la tatu la Dunia kama taifa huru na wako Kundi G pamoja na Brazil, Cameroon na Uswizi.

Dusan Tadic atakuwa nahodha wa kikosi cha Qatar, huku wachezaji kama Dusan Vlahovic, Luka Jovic na Sergej Milinkovic-Savic pia wamejumuishwa kwenye kikosi cha Stojkovic.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa