Kocha wa Ghana Otto Addo amekasirishwa na uamuzi wa kuwapa Ureno penalti katika ushindi wao wa kusisimua dhidi ya Ghana hapo jana akisema kuwa: “Sijui kama VAR haikuwa makini”.

 

 Addo: "Sijui Kama VAR Haikuwa Makini"

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika hatua za makundi katika Makombe matano ya Dunia mfululizo alipofunga bao la kwanza katika Uwanja wa 974, huku Ureno ikishinda 3-2.

Ghana, hata hivyo, walikasirishwa na uamuzi wa mwamuzi Ismail Elfath kutoa mkwaju wa penalti, wakiamini kuwa Mohammed Salisu alishinda mpira na hakumchezea rafu mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or.

Alipoulizwa ikiwa Ronaldo alifaidika na uamuzi mzuri, Addo alisema: “Nadhani itabidi uulize mwamuzi. Sina uthibitisho wa hilo, lakini tulikuwa tunacheza mpira, basi kulikuwa na mawasiliano na sijui walikuwa wanafanya nini, sijui kama VAR haikuwa makini.”

 Addo: "Sijui Kama VAR Haikuwa Makini"

Addo aliendelea kusema kuwa mchezo wa kusuasua, walifanya makosa machache kuruhusu bao la pili na la tatu, ndio tukawafungulia njia za kupita na hapo ndipo ikawa bahati mbaya kidogo.

Kwa jinsi ambavyo Ghana walivyocheza janawangeweza kupata pointi moja, mwamuzi hakuwa upande wao na kwa mtazamo wake kadi za njano ambazo walipewa walistahili lakini akilalamikia suala la yeye kushika jezi alimshangaza sana.

Addo akasema kuwa aliweza kuwauliza baadhi ya watu kutoka FIFA kama abaweza kuzungumza kwa ufupi na mwamuzi kwa utulivu, lakini wakasema yuko kwenye kikao na haiwezekani.

 Addo: "Sijui Kama VAR Haikuwa Makini"

Lakini hawakuishia hapo waliulizwa pia wachezaji wa Addo akiwemo Tariq Lamptey ambae aliingia kipindi cha pili cha mchezo na kusema kuwa hawezi kusema chochote, huku akisistiza kusema kuwa angependa kupata ushindi kwenye michuano hiyo.

Timu za Afrika 5 ambazo zimeingia kwenye Kombe la Dunia hakuna ambae amepata pointi 3 kwenye mechi yake ya kwanza ya ufunguzi ambapo, Tunisia na Morocco wao wamepata sare wakati kwa upande wa Senegal, Cameroon na Ghana wmaepoteza mechi zao za kwanza.

 Addo: "Sijui Kama VAR Haikuwa Makini"


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Addo, Addo: “Sijui Kama VAR Haikuwa Makini”, Meridianbet

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa