Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michuano mitano tofauti ya Kombe la Dunia baada ya kufunga bao la kwanza jana akiwa na Ureno walipokuwa wakimenyana dhidi ya Ghana.

 

Ronaldo Azidi Kuweka Historia Kombe la Dunia la Tano

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 alipachika bao hilo kwa mkwaju wa penalti katika kipindi cha pili na kuifanya Ureno kuongoza huku Ghana nao wakifanya mashambulizi ya kutafuta bao la kusawazisha.

Hilo lilikuwa bao la nane la Ronaldo katika Kombe la Dunia, ambapo akiwa amefunga kila hatua ya makundi wanayoingia na kufanya hivyo zaidi ya mchezaji yeyote katika hatua hizi.

Pele, Uwe Seeler na Miroslav Klose wote wametikisa nyavu kwenye Fainali nne za Kombe la Dunia lakini Ronaldo sasa yuko mbele katika suala hilo baada ya kufunga kwenye fainali ya tano.

Stats Perform inaangalia kila moja ya mabao saba ya awali ya Ronaldo kwenye hatua kubwa kuliko yote, matatu kati ya hayo yalipatikana katika mchezo mmoja, ambapo mwaka 2006 alifunga kwa mkwaju wa penati bao la kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia walipocheza dhidi ya Iran na kushinda 2-0 huko Frankfurt Ujerumani.

Ronaldo Azidi Kuweka Historia Kombe la Dunia la Tano

Baada ya kufunga bao hilo dhidi ya Iran aliweka rekodi ya kuwa ni mchezaji mwenye umri mdogo zaidi wa Ureno kuwahi kufunga katika mashindano hayo akiwa na miaka 21 na siku 132, rekodi ambayo ipo hadi sasa, licha ya Ureno kumaliza nafasi ya tatu mwaka huo na hakuongeza idadi ya mabao yake.

Mwaka 2010 michuano hiyo ilifanyika Afrika Kusini na Ureno waliipasua Korea Kaskazini kwa mabao 7-0, huku Ronaldo akifunga bao la sita na kumaliza kipindi cha miaka miwili cha kungoja bao la Kimataifa. Ureno ilishindwa kufumania nyavu katika mechi yoyote kati ya tatu nchini Afrika Kusini na wakatolewa katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Kombe la Dunia la mwaka 2014 lililofanyika Brazil, Ureno walipocheza na Ghana na kushinda 2-1, Ronaldo alifunga bao la ushindi dakika za lala salama katika mechi ya mwisho ya kundi la Ureno lakini haikutosha kuizuia timu yake kuondoka Brazil mwaka huo katika raundi ya kwanza nyuma ya Marekani na washindi wa michuano hiyo Ujerumani.

Ronaldo Azidi Kuweka Historia Kombe la Dunia la Tano

Lakini pia mchezaji huyo hakuishia hapo, Kombe lilofuata lilipigwa nchini Urusi 2018 ambapo kwenye mechi yao dhidi ya Hispania iliyoisha kwa 3-3, Ronaldo aliingia kwenye michuano hiyo akiwa mchezaji bora wa Dunia alifunga hat-trick na kufanya kuwa moja ya maonyesho bora ya muda wote ya Kombe la Dunia la mtu binafsi baada ya kufunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati, bao la pili alifunga kwa kupiga shuti kali ambalo lilimshinda David De gea, bao la tatu akafunga kwa mkwaju wa faulo.

Mchezaji huyo aliweza kupachika bao kwenye mechi yao dhidi ya Morocco huko Moscow Urusi 2018 walipokuwa wakiumana dhidi ya Ureno waliposhinda kwa bao 1-0 huku Cristiano akitupia bao kambani, lakini walipomenyana dhidi ya Uruguay hakuweza kufunga na wakapoteza kwa mabao 2-1 katika hatua ya 16 bora.

Ronaldo Azidi Kuweka Historia Kombe la Dunia la Tano

Kwahiyo kwa kufunga jana Cristiano anaweka historia kwa kufunga bao kwenye kila Kombe la Dunia kwenye hatua ya makundi wanayoingia akianzia 2006, 2010, 2014, 2018 na 2022 mfululizo.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Ronaldo, Ronaldo Azidi Kuweka Historia Kombe la Dunia la Tano, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa