Kocha mkuu wa Morocco Walid Regragui ameipongeza timu yake kwa kufanya nchi na Afrika kujivunia lakini amekubali mambo yaliyoifanya Ufaransa kutinga fainali ya Kombe la Dunia.

 

Regragui Amesema Morocco Imeiheshimisha Afrika

Morocco ambao ndio Waafrika wa kwanza kufuzu nusu fainali ya Kombe la Dunia, huku wakijizatiti kupata matokeo dhidi ya mabingwa watetezi wa Didier Deschamps, ingawa walichapwa kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Al Bayt.

Theo Hernandez na Randal Kolo Muani ndio walifanya ubao wa matokeo ukasoma tofauti kati yao na Ufaransa huku vijana hao wa Didier wakijiandaa na fainali dhidi ya Argentina ya Lionel Messi siku ya Jumapili.

Regragui aliangazia kampeni ya kihistoria sio Morocco pekee bali bara zima baada ya kuzishinda Ubelgiji, Uhispania na Ureno kuelekea kuangukia pungufu katika mechi nne zilizopita akisema kuwa;

Regragui Amesema Morocco Imeiheshimisha Afrika

“Tuligundua tumepata mafanikio makubwa tayari, tunajua kwamba vyombo vya habari vilituunga mkono na kwenye TV, tuliona jinsi kila mtu alivyokuwa na fahari, tumekatishwa tamaa, tulitaka kuweka hai ndoto ya watu wa Morocco. Tutahitaji kutafakari kushindwa huku, lakini tumefurahishwa na kile tulichokipata na tulihisi tungeweza kwenda mbali zaidi.”

Regragui anasema kuwa aliwaambia wachezaji anajivunia wao, Morocco nzima inajivunia wao na Dunia pia inajivunia kwani walifanya kazi kwa bidii na walicheza kwa bidii, walicheza soka la uaminifu na hilo ndilo walitaka kufanya.

Simba wa Atlas walitoa taswira nzuri ya nchi yao na Afrika, ikiwakilisha nchi yao na bara lao, walienda mbali walivyoweza kwenye mashindano na hilo ni kubwa, lakini walilazimika kufanya vizuri katika siku zijazo.

Regragui Amesema Morocco Imeiheshimisha Afrika

“Tunapaswa kufanya hivyo mara kwa mara ikiwa tunataka kuwa kwenye ramani ya soka. Huenda tusiwe wazuri kama Uhispania, Brazil au Uingereza, lakini ninataka kufuzu kwa kila mashindano.”

Morocco walikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa na asilimia 60-70, lakini hata hivyo walitinga nusu fainali. Walitaka kuandika upya vitabu vya historia, lakini hawawezi kushind aKombe la Dunia kwa miujiza, kwani unahitaji kufanya kazi kwa bidii na hilo ndilo wataendelea kufanya.

Hakuishia hapo ameongelea pia mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu ambayo watamenyana dhidi ya Croatia siku ya Jumamosi, na akaapa kuwa Morocco itapigana tena, ingawa anaweza kutoa nafasi kwa wale ambao hawajashiriki mara nyingi nchini Qatar.

Regragui Amesema Morocco Imeiheshimisha Afrika

“Baada ya kushindwa namna hii, huwa ni vigumu kupanga siku zijazo. Tutakuwa na muda wa kupona, na kisha tutajaribu kuifanya nchi yetu kuwa na kiburi na kushinda nafasi hiyo ya tatu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa