Cristiano Ronaldo anatumai kuwa anaweza kuwa mtu wa kumshinda Lionel Messi katika Qatar 2022, lakini haamini kwamba ushindi wa Kombe la Dunia kwa Ureno utamaliza mjadala wa soka kuhusu Messi.

 

Ronaldo: "Ushindi wa Kombe la Dunia Hautamaliza Mjadala wa Messi"

Ronaldo na Messi ndio magwiji wawili wa kisasa wa mchezo huo, huku wafuasi wa kila mchezaji wakidai kuwa wao ndio bora zaidi wakati wote, Lakini licha ya mafanikio ya Ubingwa kwa Euro na ushindi wa mwaka jana wa Argentina katika Copa America, hakuna kati yao aliyewahi beba Kombe la Dunia.

Ronaldo amevumilia msimu mgumu katika klabu ya Manchester United, lakini amewasili Qatar akiwa na hali ya kujiamini, hata kama haamini kwamba ana lolote la kuthibitisha katika yale yanayoendelea.

Ronaldo amesema kuwa; “Hata kama ningeshinda Kombe la Dunia, kungekuwa na mjadala huu ni kama katika kila kitu, kuna wengine wanapenda kuongea zaidi, wengine kuongea uzushi”

Ronaldo: "Ushindi wa Kombe la Dunia Hautamaliza Mjadala wa Messi"

Yeye ni mchezaji mwenye tamaa zaidi na anasema kuwa angependa kushinda shindano hilo, lakini ikiwa hatashinda bado angefurahi kwa kila kitu ambacho amefanya hadi sasa. Kama watu wangemwambia hataweza kushinda taji hilo, angejivunia kwa ambavyo amefanya.

Cristiano anasema kuwa kushinda Kombe la Dunia ilikuwa ni ndoto kwake, na inawezekana lakini wataona anatumaini nguvu zote ziko upande wao. Kama Ureno na Argentina kila moja ikishinda kundi lake, wawili hao hawatakutana uwanjani hadi fainali ya Desemba 18.

“Ilikuwa ni kampeni ambayo nimekuwa nikifanya, ambayo nimekuwa nikiitaka kwa miaka mingi, nimetimiza ndoto ya kuweza kuifanya na itakuwa Kombe langu la tano la Dunia. Nina umakini na nina matumaini makubwa kwamba mambo yatakwenda vizuri”

Ronaldo: "Ushindi wa Kombe la Dunia Hautamaliza Mjadala wa Messi"

Mchezaji huyo pia hakusita kuongelea kuhusu yeye na Messi kuonekana wote wamepiga picha wakiwa wanacheza mchezo wa Chess na kusema kuwa; “Checkmate sisi kufanya katika maisha, si tu katika chess. Na mimi kufanya hivyo mara nyingi”

Mchezaji huyo anasema kuwa angependa kuwa mtu wa kumuangalia Messi na itakuwa nzuri kutokea, tayari imefanyika katika mchezo wa Chess na katika soka itakuwa nzuri zaidi.

Ronaldo: "Ushindi wa Kombe la Dunia Hautamaliza Mjadala wa Messi"

Ronaldo na Messi wamekutana mara mbili pekee katika viwango vya Kimataifa, huku Ureno na Argentina wakishinda mechi moja ya kirafiki.


Kombe la Dunia Linatimua Vumbi huko Qatar ni timu 32, sawa na mechi 64 zitapigwa kwenye viwanja tofauti. Meridianbet wana uwanja wao wa Kushiriki na wewe wakati Michuano hii inaendelea. Uwanja wa Machaguo Spesho ni Kwa ajili yako, wewe Bingwa wa Kubeti. Unaweza kubeti ni Timu gani itachukua Ubingwa, Timu gani Itaongoza kuwa na kadi nyingi za Njano na Nyekundu, au Timu gani itatoka mapema kwenye michuano hiyo. Uamuzi ni wako. Chaguo ni lako. Hii ipo mpaka mwisho wa Kombe la Dunia.

BONYEZA HAPA

 

 

Ronaldo, Ronaldo: “Ushindi wa Kombe la Dunia Hautamaliza Mjadala wa Messi”, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa