Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland aipa ushindi timu yake hapo jana ambapo alirejea kwa kuiandama timu yake ya zamani Borrusia Dortmund kwa kuifunga bao la sarakasi(Acrobatic) huku City ikitoka nyuma na kupata ushindi mgumu wa 2-1 kwenye uwanja wa Etihad.

 

Haaland Aipa Ushindi City

 

Haaland ambaye amefunga wastani wa bao moja kwa kila mechi kwenye Ligi ya Mabingwa wakati wa kipindi cha miaka miwili huku Dortmund. Jana alikutana na krosi nzuri ya Cancelo katika dakika ya 84 na kuihakikishia ushindi timu yake hiyo .

Manchester city walionekana kukaribia kushindwa baada ya kufungwa goli la kushtukizwa na Borrusia kupitia kwa Jude Bellingham lakini kutokana na mashambulizi makali ya City waliweza kusawazisha bao hilo kutoka kwa Stones.

 

Haaland Aipa Ushindi City

Akiwa na umri wa miaka 22 na siku 55 Haaland anakuwa ndiye mchezaji mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya ligi ya Mabingwa kufunga bao na dhidi ya timu moja kwenye shindano hilo, na ndiye mchezaji wa pili kuwahi kufanya hivyo dhidi ya Dortmund baada ya Ciro Immobile.

Safu ya ulinzi bado haijaweza kumzuia Haaland toka atue Uingereza , huku raia huyo wa Norway akiifungia City mabao 12 kabla ya mechi ya Jumatano. Matokeo hayo yanamaanisha kuwa hawajafungwa katika mechi 21 zilizopita wakiwa nyumbani wakiwa wameshinda 19 na sare 2, mlolongo mrefu zaidi kama huo kwa timu ya Uingereza tangu Chelsea alipoweka rekodi hiyo mara 21 kati ya Septemba 2006 na Desemba 2009.

 

Haaland Aipa Ushindi City

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa