Kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter ameapa na kuseam kuwa Chelsea “Itaimarika” mara watakapofanyia kazi mambo madogo madogo baada ya kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Salzburg katika mchezo wake wa kwanza toka akabidhiwe timu hiyo.

 

Potter Aapa Chelsea Kuwa Bora

Chelsea walitangulia kupata goli hapo jana kupitia Raheem Sterling katika dakika 48 na hilo ndilo lilikuwa jaribio lao la kwanza kulenga lango. Hata hivyo The Blues walifanya majaribio mengi ya kutaka kupata mabao zaidi na ndipo wakarudishwa nyuma dakika 15 kabla ya mchezo kumalizika wakati Noah Okofar aliposawazisha bao hilo kutokana na makosa ya Thiago Silva.

Kikosi cah Potter kilimalizika mchezo huo pale Stamford Bridge na asilimia ya 72 ya umiliki wa mpira na walikuwa na mashuti 17, lakini ni manne kati ya hayo pekee yaliyolenga lango. Lakini licha ya sare hiyo waliyoipata Potter alifurahishwa na jinsi wachezaji wake walivyojituma uwanjani; Alsema,

 

Potter Aapa Chelsea Kuwa Bora

“Tumesikitishwa na matokeo. Nilidhani wachezaji walitoa kila kitu.”Aliambia BT Sport . Tulifunga bao zuri lakini tulipoteza kidogo kipindi cha pili. Kipa wao ameokoa vyema, ndivyo ilivyo, lazima tujitafute wenyewe.

Potter aliongezea kwa kusema kuwa siku zote kuruhusu bao kunakera  na safu ya ulinzi ilikuwa bora kwa ujumla ni maelezo madogo tu ambayo yanatakiwa kuboreshwa. Chelsea mechi ya kwanza alichapwa bao 1-0 na Dinamo Zagreb na ndio mechi iliyomfukuzisha Thomas Tuchel, na sasa baada ya kutoa sare jana anakuwa na alama 1 kwenye kundi ambapo ndio anashika mkia huku kinara wa kundi hilo akiwa AC Milan mwenye alama 4.

 

Potter Aapa Chelsea Kuwa Bora

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa