Graham Potter kocha mpya wa klabu ya Chelsea yenye maskani yake jijini London ameomba radhi kwa mashabiki wa timu yake ya zamani ya Brighton and Hove Albion.

Kocha huyo alietambulishwa klabuni hapo siku ya alhamisi na kusaini kandarasi ya miaka mitano na kua mrithi rasmi wa kocha aliepita klabuni hapo Thomas Tuchel.

graham potterMwalimu huyo wa sasa wa klabu ya Chelsea ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa klabu yake ya zamani akisema “Hii imekua miaka mitatu ya ajabu na ambayo imebadilisha maisha yangu na ninataka kuchukua muda mfupi kuwaaga ninyi wote ambao mmefanya kipindi hichi kua maalumu cha maisha yangu”.

“Ninaaga klabu kubwa na ambayo imekua muhimu kwangu na familia yangu.Kwa wengine natambua mabadiliko yanayokuja ghafla yanayokuja kwenye soka inakua ngumu kubadilika.

“Huenda nisiweze kuwashawishi nyote ninyi kunisamehe kuondoka lakini ningependa kuchukua nafasi huu kusema asante”.

Aliongeza kocha huyo “Natumai mtaelewa katika hatua hii ya kazi yangu,nilifikiri lazima muda ufike nishike fursa mpya.

Akamaliza kwa kuwashukuru viongozi wa klabu hiyo kuanzia ngazi ya juu mpaka ngazi za chini pia bila kusahau benchi lake la ufundi alilofanya nalo kazi kwa miaka mitatu aliyodumu klabuni hapo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa