Inaripotiwa kuwa uhamisho mkubwa wa kwanza wa Chelsea chini ya kocha mpya Graham Potter utakuwa ni wa mlinzi wa Red Bull Salzburg Josko Gvardiol, baada ya timu hiyo kukatiliwa ofa ya pauni milioni 77 kabla ya tarehe ya mwisho wa usajili.

 

Potter Anamlenga Gvardiol Januari

Gvardiol ambaye bado kijana mdogo akiwa na umri wa miaka 20 bado hana uzoefu mkubwa, akiwa tayari amepewa mechi kumi za kimataifa za Croatia pamoja na kucheza mechi 47 za klabu katika mashindano yote msimu uliopita akiwa Leipzig.

Mchezaji huyo alikuwa ni mojawapo ya mabeki ambao walikuwa wakiuliziwa sana na Chelsea na mwishoni Chelsea wakaishia kuwanunua Wesley Fofana kutoka Leicester, pamoja na Kalidou Koulibaly kutoka Napoli.

 

Potter Anamlenga Gvardiol Januari

Lakini kutokana na Koulibaly kuwa na umri wa miaka 31 na Thiago Silva kuwa na miaka 37 ni vyema kuwa watu wakawajua warithi wao mapema kuliko baadae. Beki huyo anatarajiwa kusajiliwa Januari kama itawezekana kutokana na bajeti iliyopo ambapo Potter ataruhusiwa kutumia katika dirisha la Januari, ikizingatiwa kuwa usajili wa hivi majuzi ulikuwa chini ya mwongozo wa Thomas Tuchel.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa