Chelsea the blues klabu kutoka katika jiji la London inaonekana bado inachechemea licha ya kufukuza kocha wiki moja iliopita wameweza kupata suluhu katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya.

Chini ya Mwalimu mpya Graham Potter klabu hiyo imepata sare katika dimba lao la nyumbani dhidi ya timu ya Red Bull Salrzburg ya nchini Austria katika mchezo wa wa pili wa kundi E baada ya mchezo wa kwanza klabu ya Chelsea wakipoteza ugenini dhidi ya Dinamo Zagreb mchezo uliopelekea aliekua mwalimu wa timu Thomas Tuchel kufukuzwa.

chelseaMpaka kumalizika mchezo wa jana wababe hao wa London wamevuna jumla ya alama moja wakiwa wanashika mkia katika kundi hilo linaloongozwa na klabu ya Ac Milan ya nchini Italia.

Mchezo unaofuata ni Chelsea dhidi ya Ac Milan katika dimba la San siro na ni mchezo muhimu zaidi kwa wababe hao kutoka jijini London ili kufufua matumaini ya kuwezakusonga mbele kwenye kundi hilo ambapo mpaka sasa wao wakionekana kushika mkia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa