Leonardo Bonucci nahodha wa klabu ya soka ya Juventus ameonesha kushtushwa na matokeo mabaya wanayopata klabu hiyo kwasasa.

Klabu hiyo imekuwa na kiwango cha kusua tangu kuanza kwa msimu huu wakiwa wameshinda michezo miwili pekee kwenye michezo yote waliyoshikiriki ya kimashindano msimu huu na hii imekuja baada ya kupoteza mchezo wa jana wa ligi ya mabingwa ulaya wakiwa nyumbani na kufungwa mabao mawili kwa moja na klabu ya Benfica kutoka nchini Ureno.

leonardo bonucciKatika mchezo huo ambapo mashabiki wa klabu hiyo ambao waliwazomea wachezaji wa timu hiyo baada ya kupoteza mchezo na nahodha wa klabu hiyo kusema “Tumestahili dhihaka hii na tunahitaji kubadilisha hii hali hii iliopo sasa Bonucci alisema”.

Hii inakua mara ya kwanza kwa vibibi vizee hao wa Turin kupoteza michezo miwili mfululizo za hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa ulaya tangu 1972.

Huku presha ikiwa kubwa sana kwa kocha wa timu hiyo massimiliano Allegri mashabiki wengi wakihitaji kocha huyo aachie timu hiyo kutokana na muenendo wa timu hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa