Henock Inonga Baka beki wa kimataifa wa Congo anayeitumikia klabu ya Simba inayoshirki ligi kuu ya Tanzania bara amefanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Congo kitakachoenda kushiriki mechi mbili za kirafiki dhidi ya Burkina Faso pamoja na Sierra leone.

Inonga anakua mchezaji pekee kuitwa timu hiyo ya taifa anayecheza katika ligi kuu ya Tanzania bara licha ya kua na wachezaji wengi wanaocheza ligi hii kutoka taifa hilo na wenye uwezo pia lakini anabahatika kuitwa kwenye kikosi hicho chini ya mwalimu Sebastian Desabre.

inonga, Inonga Aitwa Timu ya Taifa ya Congo., MeridianbetBeki ambaye amekua na kiwango bora sana tangu akiwa klabu ya Dc Motema Pembe huku akifanikiwa kua mchezaji bora wa msimu kwenye msimu 2020/21 baada ya kuja Tanzania anafanikiwa kua beki bora kwenye msimu wa mwaka 2021/22 hivo inaonesha ni kwa namna gani beki huyo anastahili kuitwa kwenye timu hiyo ambayo imejaza wachezaji wengi wanaocheza vilabu mbalimbali barani ulaya.

Pia hii inaonesha ligi kuu ya Tanzania ni kwa kiasi gani inaendelea kukua kwa kasi kutokana na kutoa wachezaji wenye ubora wanaoweza kuitwa katika zao za taifa ambazo zina ushindani mkubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa