Pep Guardiola kocha wa klabu ya Manchester City na mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza amesifu uwezo wa kiungo Borussia Dortmund Jude Bellingham.

Katika mchezo uliopigwa katika dimba la Etihad usiku wa kuamkia leo kati ya Man City dhidi ya Dortmund ukiwa mchezo wa pili wa hatua ya makundi kiungo huyo raia wa Uingereza alikua na kiwango bora na kufunga bao pekee la Dortmund katika mchezo huo kilichomfanya kocha huyo kusifu uwezo wa kiungo huyo raia huyo wa Uingereza.

Pep anasema “Jude ni mchezaji wa daraja la juu na ni mchezaji mkubwa pia na sio kwasababu kocha wa Manchester City kasema hapana hili kila mtu analijua”.

pep guardiolaKatika mchezo ambapo klabu ya Dortmumd ambao walianza kupata bao kupitia kwa Jude Bellingham kabla ya Man City kutoka nyuma na kushinda mabao mawili kwa moja magoli ya beki kitasa John Stones kabla Earling Haaland kuhakikisha ushindi kwa vijana hao wa Pep.

Kitu kilichovutia zaidi kwenye mchezo huo ni Haaland kukutana na timu yake ya zamani na kuifunga lakini aina ya bao pia alilofunga likiwaacha watu midomo wazi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa