Massimiliano Allegri kocha wa klabu ya Juventus ya nchini Italia ameonesha kutokuogopeshwa na kukosa kibarua chake ndani ya klabu hiyo licha ya matokeo mabaya timu hiyo inayopata kwasasa.

Kocha huyo amewataka watu kutokuhofia kuhusiana na kipigo timu yake ilichokumbana nacho katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya usiku wa kuamkia jana dhidi ya klabu ya Benfica ya nchini Ureno.

allegriIkumbukwe klabu ya Juventus haina hata alama moja kwenye michuano hiyo ya ulaya baada yakupoteza michezo yote miwili ya kwanza pamoja na ugumu wote wanaopitia klabu ya Juventus Allegri anaamini yeye ndo mtu pekee wa kuivusha klabu hiyo katika wakati mgumu iliokua nao kwasasa.

“Ndio kabisatuna ugumu kidogo japo kuna wachezaji wachache wanakosekana “Alijibu kocha huyo akiwa anahojiwa na chombo kimoja cha habari huko nchini Italia alipoulizwa kama anaweza kubadili hali ya hewa na kuongeza “Lazima tufanye kazi wote na ni wajibu wa wote”

Kocha huyo anaamini hata wangepata sare kwenye mchezo wa jana bado yangekua matokeo mabaya hivo huu ni muda kujitazama wanakosea wapi ili warekebishe kuelekea michezo mingine ili warudi kwenye njia ya ushindi na kurusisha ubora wao.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa