Giovanni van Bronckhorst kocha wa klabu ya Rangers ya nchini Uskochi amedai matokeo waliyoyapata dhidi ya klabu ya Napoli katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya wakiwa nyumbani hauoneshi uhalisia wa wao walivyocheza.

Timu hiyo kutoka nchini Uskochi imepoteza kwa magoli matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Napoli ya nchini Italia magoli ya Napoli yakifungwa na Matteo Politano, Raspadori, pamoja Tanguy Ndombele aliefunga goli la tatu katika mchezo huo mapema kabisa Piotr Zielenski akikosa mkwaju wa penati.

van bronckhorst“Tulicheza vizuri na kujipanga vizuri kabla ya kupunguzwa na kua kiwanjani, Nilijua mchezo utakua mgumu baada ya kupunguzwa idadi kiwanjani lakini wachezaji walijitoa kwa kila kitu ili kupata matokeo mazuri”

Rangers walicheza wakiwa pungufu kwa takribani dakika 30 za mchezo huo baada ya mlinzi wao James Sands kupata kadi nyekundu mnamo dakika ya 55 ya mchezo huo.

“Nilipenda ushindani baina yetu na Napoli kabla ya kupewa kadi nyekundu kwa mchezaji wetu” alidai kocha huyo wa raia wa Uholanzi.

Rangers wanabaki wanashika mkia kwenye kundi A baada ya kupoteza michezo yote miwili ya awali hivo wakiwa wana kazi ya ziada ya kufanya ili kusonga mbele katika michuano huku mchezo wa tatu wakisafiri kuelekea Anfield kukipiga na klabu ya Liverpool.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa