Allegri: Sifahamu Kama Dyabala Atasalia Juventus!

Massimiliano Allegri anasema kuwa hana uhakika ikiwa nyota wa Juventus Paul Dybala atasalia klabuni hapo zaidi ya msimu wa joto, licha ya kucheka na nyavu kwenye ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Salernitana.
Allegri: Sifahamu Kama Dyabala Atasalia Juventus!
Paulo Dybala

Staa huyu amefunga magoli nane msimu huu akiwa na Juventus, sawa na Alvaro Morata, na zaidi ya wachezaji wengine kikosini hapo. Hata hivyo, hii bado haijamuweka mbali na kuhusishwa na uhamisho klabuni hapo.

Akizungumzia hali hii, bosi wa Juventus, Massimiliano Allegri amesema kuwa hafahamu ikiwa staa huyu ataendelea kuwepo baada ya msimu huu wa joto.

“Sifahamu ikiwa ataendelea kuwa mchezaji wa Juventus au la! Ndiyo maana tuna klabu na mimi nipo katika mstari huo. Sio Paulo [Dybala] pekee mkataba wake unakaribia kuisha, pia kuna Cuadrado ma Bernardeschi na De Sciglio” – Massimiliano Allegri

“Kwa upande wangu, na kwa upande wa timu, kuna suala la nia ya kufanya vizuri pekee. Ninafanya tathmini ya wachezaji, lakini kuna mawala mengi ikiwa ni pamoja na masuala ya mkataba yanayopaswa kutazamwa.” Massimiliano Allegri

Dybala amekuwa na vipindi tofauti klabuni hapo akiwa na nafasi ya kutambuliwa kama mchezaji muhimu sana Juventus, amekuwa akihusishwa na nia ya Liverpool kumsajili.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe