Aishi Salum Manula ndio jina lililotajwa zaidi usiku wa jana na asubuhi ya leo tarehe 21,03,2022. Na itabaki kwenye kumbukumbu za watu wengi kua Manula kwa usiku wa jana ndio mwamba aliyeziba matundu ya kikapu kilichojazwa magoli cha Asec Mimosas pale Stade de L’amitie nchini Benin,
Ndio nchini Benin, na hii ni kwakua nyumbani Ivory Coast ambako ndiko Asec inatoka kuna ukarabati wa viwanja vya soka na kupelekea mchezo huu kuchezwa Benin ambako kiufupi ni kwamba Asec alikua mgeni mwenye Uwenyeji kiutarabu, Hili si lakuangalia sana kwa sasa kubwa ni matokeo ya simba dhidi ya Asec na nini wanaweza kufanya kupindua meza na kufuzu hatua ya robo fainali kombe la shirikisho.
Simba ilipoteza mchezo wao dhidi ya Asec Mimosa kwa kufungwa magooli matatu kwa nunge 3:0 magoli yaliyofungwa na Aubin Koame dakika ya 16, Stephane Aziz Ki dakika ya 25, karim Konate dakika 57, Asec walipata Penati mbili zote hazikufua dafu mbele ya mlinda mlango Aishi salum Manula.
Simba atasubiri mechi yake ya mwisho pale Lupaso (Benjamin Mkapa Stadium ) dhidi ya Union Sport Gendarmerie Nationale na atalazimika kupata matokeo kwenye mechi hiyo ili aweze kufuzu hatua ya robo fainali.
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.