Hilton: 'Huwa Ninasahau Kama Nina Miaka 42'

Mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa nyongeza, mlinzi wa klabu ya soka ya Montpellier mwenye umri wa miaka 42, Vitorino Hilton amefunguka na kusema kuwa ana sababu zake za kudumu katika soka namna hiyo.

Mshindi huyo mara mbili wa Ligue 1 Conforama aliiambia RMC: “Unatakiwa kufanya mazoezi kila siku. Ninajiandaa katika njia maalum kiasi kwamba huwa ninasahau umri wangu wa sasa. Ninauweka pembeni kabisa. Wakati mwingine ninasahau kabisa kama nina umri wa miaka 42 na ninacheza na mtu kama Joris Chotard ambaye ana umri wa miaka 18. Ninadhani kwamba jambo hilo linanisaidia sana kujisikia fiti na kujitoa hasa uwanjani.

β€œMiaka minne iliyopita nilidhani ya kwamba mke wangu atanisihi niache kucheza soka.”

β€œMiaka minne ama mitano iliyopita mke wangu aliniambia niache kucheza soka kwa muda huo. Kwa sasa yupo hapa pembeni yangu akinipa sapoti kubwa sana na ananiambia kuwa nisichoke, niendelee. Inanipa moyo sana na nguvu zaidi. Upendo wangu kwenye soka bado upo moyoni mwangu. Ninaipenda soka tangu nikiwa mtoto mdogo kabisa. Na ninadhani kuwa nitaendelea kuipenda soka hivi hivi na nina ari kubwa ya kucheza mpira wa miguu.”
Kwa sasa Hilton ameongeza muda wa miezi 12 mbele wakati ambapo Souleymane Camara, mwenzake wa klabu moja waliyoipa mafanikio na kutwaa taji mwaka 2012 wakiwa na Montpellier, yupo anakula bata zake kwenye boti akiwa na umri wa miaka 37 tu!

β€œNinapenda sana kucheza!”

Hilton anasema kuwa: Nilikuwa na kocha nikiongea naye ambapo tulizungumza sana na kisha nikaongea na Mkurugenzi wa Michezo, Bruno Carotti. Nilimpa mawazo yangu ya kupenda kuendelea kucheza soka. Wiki moja mbele Rais ainitumia ujumbe akinitaka nirudi klabuni. Tulizungumza kwa dakika 20 na kisha nikasaini mkataba wa nyongeza. Ni rahisi sana, ninapenda sana kucheza kabumbu!”

39 Komentara

    kimasihara anaweza fikia record ya rivaldo

    Jibu

    Safi. Fundi wa Mpira#meridianbettz

    Jibu

    Fundi wa mpira asiyekuwa na makuu#meridianbettz

    Jibu

    Hahahaha anazingua huyo anasahau vipi miaka yake sasa duuh

    Jibu

    Huyo mpira uko damuni ata akifika miaka 50 yuko tayar ata aende timu za wazee

    Jibu

    Fundi wa mpira huyo

    Jibu

    Namkubali Ni fundi mzuri

    Jibu

    Bado uwezo anaa sanaa

    Jibu

    Inaonesha uwezo wake bado anao na anajituma sana uwanjani

    Jibu

    Mwenye mpira hana neno katika sekta iyo namkubal sana πŸ’ͺ

    Jibu

    Fresh tu

    Jibu

    bado yupo vizuriii

    Jibu

    Duuh ni hatari mpira uko kwenye damu yupo kama mm na meridian

    Jibu

    Anazeeka na ujuzi wake

    Jibu

    Hilton anajua Sana mpira

    Jibu

    Fundi wa mpira huyo

    Jibu

    Safii sana Fundi mpira huyo

    Jibu

    Bado yuko fitii sana akazane tu

    Jibu

    Anajua mpira sn

    Jibu

    Safi sana Hilton kama una uwezo wa kufanya kazi ,fanya kazi baba usiangalie umri bado unadai mbona ,na wanawake tunatakiwa kuwaunga mkono wanaume tulionao ili wajitahidi katika kutafuta kipato kama anavyofanya mke wa Hilton.

    Jibu

    gud newz asante

    Jibu

    bado yuko vizuri cha msingi mazoezi ya nguvu atadumu katika soka pamoja na umri wake

    Jibu

    sawa bwana hilton mazoezi yanakusaidia ndio maana haujui umri wako

    Jibu

    Umri sio tatizo ki kubwa mpira bado anaucheza

    Jibu

    Safi sana hilton..!bado tunajifunza kupitia wew

    Jibu

    Yupo vizuri Sana ndo maana hazeeki

    Jibu

    Kwa league za. Wenzutu huu umri ni mkubwa sanaa kuendelea kukipiga kwenye soka

    Jibu

    Bado yuko vizuri kwenye mpira

    Jibu

    Hilton jembee#meridianbettz

    Jibu

    Mpira upo kwenye damu

    Jibu

    Uwezo wake ndo upo juu haichuji so lazma bado ajione anasafar ndev kweny soka

    Jibu

    Hata mie mmewangu Anamiaka 50 lakin sijawahi mkataza kucheza huko SPAIN #Meridianbettz

    Jibu

    Kazi na umri

    Jibu

    Pongezi kwako Hilton

    Jibu

    Umri umeenda Hadi anasahau miaka yake

    Jibu

    Hahahahaha ni story nzuri #Meridianbettz

    Jibu

    Duh yup vzr sana thnks meridian bet tz

    Jibu

    Yuko vizur

    Jibu

    Anatisha

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.