Mshambuliaji wa Napoli, Lorenzo Insigne amekubali kujiunga na klabu ya Toronto inayoshiriki ligi kuu ya MLS nchini Canada kuanzia majira ya kiangazi mwezi Julai.

Toronto FC wamekubaliana na Lorenzo Insigne ambaye mkataba wake na klabu ya Napoli unakamilika mwishoni mwa msimu huu na tayari amekubali mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo.
Insigne amekubali mkataba wa €11.5 million (£9m/$13m) kwa mwaka pamoja na bonasi kwa kipindi cha miaka mitano (5) na mchezaji huyo mwenye miaka 30 anajiandaa kuondoka kuelekea canada Julai 1 mkataba wake utakapokamilika.
Lorenzo amekulia Napoli akitokea akademi na kupandishwa timu ya wakubwa ambapo amecheza mechi 414 mpaka sasa akiwa amefunga jumla ya magoli 114.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.


