Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Pamba kwa bao 1-0, kikosi hicho  cha Ken Gold kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Gwambina.

 

 

Ken Gold Yaanza Tizi

Mchezo huo wa michuano ya Championship ulipigwa Septemba 17 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nyamagana, Jijini Mwanza.

Akizungumzia maandalizi yao, Katibu Mkuu wa Ken Gold, Benson Mkocha amesema kuwa “Tunamshukuru Mungu kikosi kimeanza mazoezi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Gwambina.

“Licha ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Pamba lakini wachezaji wamelisahau hilo na wameahidi kwenda kupambana kwenye mchezo ujao ili waweze kupata matokeo.”

 

Ken Gold Yaanza Tizi

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa