Mwenyekiti Gwambina Aachia Ngazi.

 

Mwenyekiti wa Gwambina FC, Omary Mmasi amejiuzuru nafasi hiyo huku ikiwa haijatajwa sababu za kiongozi huyo kung’atuka.

Gwambina ambayo inashiriki Ligi Kuu kwa msimu wake wa kwanza inahaha sana kukwepa rungu la kushuka daraja kwani hadi sasa imekusanya pointi 31 na kukaa nafasi ya 17.

Afisa habari wa timu hiyo, Felician Mwenzi, amethibitisha uongozi kupokea taarifa hiyo huku akisema ni masikitiko makubwa ikizingatiwa timu haipo sehemu salama.

“Ni kweli tumepata taarifa hizo lakini ni masikitiko kwani tupo katika mapambano makali kwa kipindi hiki kigumu tukisaka matokeo mazuri” amesema Mwenzi


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 Komentara

    Mhhh

    Jibu

    Dah ni balaa sana gwambina

    Jibu

Acha ujumbe