Mawakala wa Olivier Giroud wamekutana na Milan tena leo kuweka mambo sawa, lakini lazima wahakikishe Chelsea inamwacha aomdoke bure au hakutakuwa na dili.

Milan alikuwa kwenye mazungumzo kwa wiki kadhaa na upande wa Giroud wakitarajia kwamba atakuwa wakala huru, lakini Chelsea ilitangaza kuwa wameanzisha kipengele cha kuongeza mkataba wake hadi Juni 2022.

Giroud Anawapa Kichomi Milan

Hiyo ilifanywa mwezi Aprili, lakini imethibitishwa mwezi huu, ikidokezwa kuwa maajenti wake wanajua vizuri hali hiyo na waliielezea Milan pia.

Ripoti nchini Italia zinaonyesha mawakala wake walihakikisha Chelsea itamwachilia bure ikiwa ofa itaingia kutoka nje, na ingeomba ada kwa klabu nyingine ya Ligi Kuu, kwa mfano West Ham United.

Kwa mujibu wa Sky Sport Italia, mawakala wake walikutana na Milan tena Jumatano na kuweka sawa maelezo ya masharti ya binafsi kwa mkataba wa miaka miwili.

Milan wanakuwa na hofu kama watamchukua Giroud akiwa wakala huru na ni juu ya wawakilishi wake kutatua hali hiyo.


 

WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa